Kuonyesha imeanza kujipanga mapema kwa ajili ya Ligi Kuu Bara msimu
ujao, Ndanda FC ya Mtwara imeomba wadau kuisaidia timu hiyo ambapo nia yao ni
kufikisha shilingi bilioni 1.3 ili ishiriki ligi vizuri.
Ndanda FC ambayo ni miongoni mwa timu tatu zilizopanda msimu huu ikiwa
pamoja na Polisi Moro na Stand United, imesema hivyo huku ikidai kwenye akaunti
yake, tayari inamiliki shilingi milioni 1.1.
Katibu Mkuu wa Ndanda, Suleiman Kachele, ameeleza kuwa wameandaa
mikakati kabambe ya kuhakikisha wanaingia ligi kuu kwa kishindo na wachezaji
wenye viwango ili kutoa ushindani mkali.
“Tunatarajia kukutana Jumamosi kwa kuwakutanisha wadau mbalimbali ili
waweze kusaidia katika bajeti yetu ambapo tunahitaji kiasi cha shilingi bilioni
moja na milioni mia tatu.
“Mpaka sasa sisi tuna kiasi cha shilingi milioni 1.1 ambacho
hakitutoshelezi, hivyo ni vyema wadau mbalimbali wakajitokeza kutusaidia kwani
tumepanga kuwatembelea watu tofauti watusaidie,” alisema.
0 COMMENTS:
Post a Comment