Juhudi za Simba kufanya mabadiliko
katika baadhi ya vipengele vya katiba yake hasa kile cha kumpa nafasi mgombea
yoyote hata aliyewahi kufungwa jela kugombea, zimekwama.
Kamati ya sheria ya TFF imekikataa kipendekezo
hicho ambacho kilikuwa kinaeleza mtu aliyewahi kufungwa na akarudi uraiani kwa
miaka mitano bila kufanya makosa anaweza kugombea.
Awali Simba ilikuwa inaficha kuhusiana
na kukataliwa kwao, lakini leo imethibitisha kuhusiana na hilo kupitia msemaji
wake, Asha Muhaji.
Ilielezwa kwamba mmoja wa viongozi walio
katika kamati za Simba alitaka kugombea uenyekiti, kutokana na uamuzi huo maana
umezima ndoto zake.
Muhaji amesema yalikuwa mapendekezo ya
wanachama na walilenga kutaka Wanasimba ambao waliingia gerezani watakuwa
wamepata mafunzo kutokana na vifungo, basi wapewe nafasi.
Vipengele vingine vimekubaliwa na kamati
hiyo ya sheria ya TFF na vimepelekwa kwa msajiri kwa ajili ya kupitishwa.
0 COMMENTS:
Post a Comment