Gumzo la uzembe wa kipa Juma Kaseja na
beki Kelvin Yondani kusababisha Yanga kufungwa na Mgambo Shooting kwa mabao
2-1, limezimwa na uongozi wa klabu hiyo.
Mashabiki na wanachama wa Yanga walionyesha kuchukizwa
na Kaseja na Yondani na kusema ndiyo waliosababisha Yanga kupoteza mchezo kwa Mgambo.
Lakini Katibu Mkuu wa Yanga, Beno Njovu
amezungumza leo na kusema uongozi hautaki kumlaumu mtu na badala yake
unaendelea kupamabana.
“Inawezekana hata Azam FC nayo
ikateleza, hivyo tunaendelea kupambana hadi mwisho wa ligi ndiyo tutajua kama
tumeshindwa au la.
“Hatupaswi kulaumiana sasa maana ni
mapema sana, hivyo tunasisitiza vita bado ni mbichi na sisi tumekuwa
tukijipanga kuendelea kutafuta ushindi.
“Hatujui wenzetu wanatumia njia gani
lakini na sisi tuna njia zetu ambazo tunatumia kwa ajili ya kupata ushindi,”
alisema Njovu.
Katika mechi hiyo iliyochezwa kwenye
Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga, Yanga ilifungwa bao la kwanza babada ya Kaseja
kushindwa kuondoa mpira aliorudishiwa na Yondani na bao la pili, Yondani
akamuangusha mchezaji wa Mgambo ndani ya eneo la hatari na kusababisha penalty.
0 COMMENTS:
Post a Comment