Castle Lager kupitia ushirikiano wake
na FC Barcelona leo imeanza zoezi la kusajili timu zitakazoshiriki shindano la
Castle Lager Perfect 6 la mpira wa miguu litakalohusisha wachezaji sita kila
upande linalofanyika kitaifa.
Akizungumza jijini Dar es salaam
jana, Meneja wa Bia ya Castle Lager, Kabula Nshimo amesema kwamba washiriki wa
shindano hilo watajiandikisha kupitia bar mbalimbali nchini na kuunda timu
ambazo zitashindana kupitia mabonanza yatakayofanyika maeneo mbalimbali nchini.
“Shindano litafanyika nchi nzima
ambapo timu mbalimbali katika Kanda saba zitasajiliwa na kucheza katika hatua
za mtoano kwenye maeneo mbalimbali ambayo yatachaguliwa na kutangazwa mapema.
Kila kanda itatoa timu moja na kufanya jumla ya timu saba ambazo zitawakilisha
Kanda hizo huku timu ya nane ikitoka kwenye vyombo vya habari. Timu hizo
zitachuana kwa mtoano kwenye robo fainali, nusu fainali, na hatimaye
fainali.
Nshimo alisema kwamba shindano hili
limelenga kuwaburudisha wanywaji wa Castle Lager na kuwapa fursa ya kucheza
soka la kujifurahisha na kufurahi pamoja. Shindano hilo litamalizika kwa kupata
washindi ambao watatembelea uwanja wa Camp Nou nchini Hispania na kujionea timu
ya FC Barcelona ikicheza katika ziara ambayo itagharamiwa kila kitu na Castle
Lager.
Aliongeza kuwa shindano la Perfect
Six limelenga kuzungumza na wanywaji wa Castle Lager ambao wana shauku ya
kucheza mpira wa miguu, kuleta pamoja wanywaji wa Castle Lager kutoka baa
mbalimbali ili wafurahie pamoja, kuongeza mauzo ya Castle Lager na kuwapa
zawadi wateja wa bia hiyo.
“Pia kupitia mashindano hayo, watu
sita watajishindia kiasi cha shilingi 100,000/= kupitia droo zitakazofanyika
kila wiki na mwisho wa kampeni itafanyika droo kubwa ambapo watapatikana
washindi wawili ambao wataambatana na na timu iliyoshinda kwenda Camp Nou
Hispania”, alisema.
Nshimo alisema kwamba timu ya
waandishi wa habari itakayoshiriki fainali za kitaifa tayari imeishapatikana.
“Katika kutambua mchango mkubwa wa vyombo vya habari, tukishirikiana na TASWA
tulizindua shindano hili kwa kuandaa bonanza la waandishi wa habari ambao
waliunda timu 8 zikashindana katika mfumo wa ligi na hatimaye timu ya Puyol
ilishinda na hii ndio timu ambayo itawawakilisha wanahabari kwenye fainali za
kitaifa zinazotarajiwa kufanyika Agosti mwaka huu jijini Dar es salaam.
Nshimo pia aliwahamasisha wanywaji wa
Castle Lager kwamba sasa kwakuwa tayari milango ya usajili iko wazi, watumie
fursa hii vizuri kuhakikisha wanashiriki katika shindano hili la kabumbu
linalotarajiwa kuleta msisimko mkubwa kama ilivyoshuhudiwa
kwenye bonanza la uzinduzi lililowahusisha wanahabari kutoka vyombo mbalimbali
vya habari hapa nchini
0 COMMENTS:
Post a Comment