Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amewapongeza marais Davor Suker na Fouzi Lekjaa
kwa kuchaguliwa tena hivi karibuni kuongoza mashirikisho ya mpira wa miguu
katika nchi zao.
Suker amechaguliwa tena kuwa Rais wa
Shirikisho la Mpira wa Miguu la Croatia (CFF) wakati Lekjaa amechaguliwa kuwa
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu la Morocco (FRFM).
Katika salamu zake za pongezi, Rais
Malinzi amesema ushindi waliopata ni uthibitisho kuwa familia ya mpira wa miguu
katika nchi zao ina imani kubwa kwao katika kuendeleza mchezo huo ndani na nje
ya nchi hizo.
Rais Malinzi amesema Lekjaa na Suker
wana uwezo wa kuendeleza kazi nzuri ambayo tayari imefanyika, lakini vilevile
kuja na mawazo mapya ambayo yatakuwa changamoto kwa ustawi wa mchezo huo nchini
Morocco na Croatia kwa ujumla.
0 COMMENTS:
Post a Comment