Mashabiki wa matawi mbalimbali ya Simba
wamekutana na kufanya kikao ambacho kwa pamoja wamekubaliana kutokwenda
uwanjani na mabango wala morali kubwa ya ushangiliaji isipokuwa kwenye mechi ya
mwisho dhidi ya Yanga pekee.
Kikao hicho
na mjadala huo vimetokana na
matokeo mabaya mfululizo ya timu hiyo kwenye mechi zake za ligi ambapo kabla ya
kikao hicho tayari uhudhuriaji wa mashabiki hao kwenye mechi za Simba
zinazopigwa katika Uwanja wa Taifa, Dar , ulishuka
maradufu ikilinganishwa na idadi ya misimu iliyopita.
Masoud Hassan
‘Ustaadh’, ambaye ni Mwenyekiti wa Tawi la Mpira Pesa
lililopo Magomeni, amesema kikao hicho kilifanyika wiki iliyopita kabla
ya mechi ya Simba na Azam iliyopigwa Jumapili.
Katika
mechi hiyo uwanjani kulikuwa na bango
moja tu la mashabiki na hakukuwa na kikundi chochote cha ushangiliaji, jambo ambalo lilizua wasiwasi mkubwa.
“Kutokana
na mwenendo mbovu wa timu,
tumekubaliana kutokwenda uwanjani na mabango yale yanayoonyesha hili ni tawi
fulani kama ilivyozoeleka, isipokuwa
tutafanya hivyo kwenye mechi tutakayocheza na Yanga pekee kwa kuwa hiyo ni mechi muhimu sana
kwetu.
“Mashabiki
wanakwenda uwanjani lakini si kwa idadi ile ya awali kwa kuwa wengi wao
wamesusa kutokana na haya matokeo. Sasa hivi tumeelekeza nguvu zetu kumuangalia
kiongozi atakayetufaa kwa ajili ya mafanikio kwenye uchaguzi unaokuja.
“Tutaanza
tena kuja na mabango msimu ujao kwa kuwa tutakayemchagua tutakuwa na imani naye
ya kuturejesha uwanjani kuishangilia timu yetu kama ilivyokuwa awali,” alisema
Masoud.
Matawi
yaliyohudhuria kwenye kikao hicho ni pamoja na Tawi la Mpira Pesa, Ubungo
Terminal, Vuvuzela, Wekundu wa Msisiri, Wekundu wa Keko na Wekundu wa Mchikichini.
0 COMMENTS:
Post a Comment