April 2, 2014


Pointi sita ambazo timu ya Mgambo JKT imezipata baada ya kuifunga Simba na Yanga, zimeisaidia kutoka mkiani mwa Ligi Kuu Tanzania Bara.


Mgambo msimu huu haijapoteza mchezo hata mmoja dhidi ya Simba wala Yanga kwenye uwanja wake wa nyumbani wa Mkwakwani.

Katika mchezo wa kwanza dhidi ya Simba Mgambo walifanikiwa kukusanya pointi tatu baada ya kushinda kwa bao 1-0, lakini pia waliishangaza Yanga juzi baada ya kuichapa mabao 2-1 kwenye uwanja huo, mechi zote zikiwa ni za mzunguko wa pili.

Katika mzunguko wa kwanza msimu huu, Simba ikiwa nyumbani ilifanikiwa kuichapa mabao 6-0 na  Yanga iliweza kuifunga bao 3-0, michezo yote ilichezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Kama Mgambo ambayo kwa sasa ipo katika nafasi ya 11 na pointi 22 ingepoteza michezo hiyo basi ingekuwa katika nafasi ya 12 ambayo ingekuwa kwenye hatari zaidi ya kushuka daraja.

Hata hivyo, siyo msimu huu tu Mgambo imekuwa ikizitesa Simba na Yanga kwani msimu uliopita ikiwa katika uwanja wake wa Mkwakwani, ilifanikiwa kutoa sare na timu zote mbili za Simba na Yanga.
Simba iliweza kutoa sare ya bila kufungana  huku Yanga ikitoa sare ya bao 1-1.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic