April 1, 2014





Chelse imetua jijini Paris tayari kuwavaa wenyeji wake PSG lakini vijana hao wa Jose Mourinho watamkosa Samuel Eto’o ambaye ni majeruhi.

Mechi hiyo ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Ulaya inasubiriwa kwa hamu na tayari kila upande umeeleza umepania kushinda.


Kutokana na kumkosa Eto’o, kocha huyo Mreno ameamua kuanza na mshambuliaji wake Mhispania, Fernando Torres.
Eto'o raia wa Cameroon ndiye amekuwa chaguo la kwanza na Mourinho na amefunga mabao 11yote kwenye uwanja wa nyumbani wa Stamford Bridge.
 Aliumia nyama katika mechi ambayo Chelsea iliibutua Arsenal kwa mabao 6-0 Machi 22.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic