Mshambuliaji mpya wa Azam FC, Didier Kavumbagu, amesema amesaini mkataba wa kuichezea timu
hiyo kwa sharti moja la kuhakikisha anafikia rekodi ya Klabu ya TP Mazembe ya DR
Congo katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika (Caf) watakayoshiriki,
mwakani.
Kavumbagu
ambaye ni raia wa Burundi, amesaini mkataba huo hivi karibuni baada ya ule wa
miaka miwili aliokuwa anautumikia akiwa na Yanga kumalizika kabla ya Azam
kumsajili yeye na kiungo mkabaji, Frank Domayo.
Akizungumza
na Championi Jumatano, Kavumbagu alisema hilo ni kati ya sharti alilopewa
katika kuipa mafanikio timu hiyo tajiri nchini baada ya kufanikiwa kutwaa
ubingwa wa ligi kuu.
Mrundi
huyo alisema Azam imemsajili maalum kwa ajili ya michuano ya kimataifa ambayo
wanaamini ataisaidia timu hiyo kutokana na uzoefu mkubwa alionao wa kushiriki
michuano hiyo.
Aliongeza
kuwa, sharti hilo la kuifikia rekodi ya Mazembe ni gumu kwake, lakini atatumia
uzoefu wake katika kuhakikisha anaifungia timu yake mabao kwa kila nafasi
atakayopata.
“Ujue
klabu yoyote inapokusajili kuna mahitaji inayoyataka kwako, ikiwemo kuipa
mafanikio ya ubingwa, ninaamini wao wameniona ninafaa, hivyo nitafanikisha
hicho wanachokihitaji.
“Itakuwa
ngumu kufikia rekodi ya TP Mazembe ya kutwaa Klabu Bingwa Afrika pamoja na
kufika fainali ya Klabu Bingwa Dunia, lakini naamini tutapambana mpaka mwisho
na tutafanikiwa,” alisema Kavumbagu.
SOURCE: CHAMPIONI
0 COMMENTS:
Post a Comment