CHOKORAA AKIWA AMEBEBWA NA MENEJA DAKOTA NA BONDIA MAARUFU NCHINI, THOMAS MASHALI |
Mwanamuziki wa Bendi ya Mapacha watatu aliyejitosa kwenye fani ya masumbwi, Khalid Chuma 'Chokoraa' usiku wa kuamkia jana (Jumapili) alimchakaza mpinzani wake, Abdul Mayenza 'Puly' kwa Knock Out raundi ya kwanza baada ya kumvizia na kumtandika kisawasawa ngumi nzito iliyomtegua bega la kushoto.
Katika
pambano hilo lililokuwa la utangulizi la raundi nne uzito wa Light Weilter lililofanyika Ukumbi wa
Friends Corner jijini Dar es Salaam, lilianza kwa kasi kila mmoja akimtupia
mwenzake makonde kuonesha hali ya kukamiana.
AKIINULIWA MKONO NA MWAMUZI BAADA YA USHINDI |
Raundi
hiyo ikiendelea Chokoraa aliyekuwa akitokea kona nyekundu alimbana mpinzani
wake kwenye kona ya bluu na kumpa ngumi nzito mfululizo zilizomfanya aonekane
kukata pumzi na kulalia kwenye kamba ya kona hiyo mpaka alipookolewa na mwamuzi
wa mchezo, Said Chaku.
Baada
ya kuokolewa pambano lilianza tena ambapo Chokoraa alimvizia tena Puly na
kumtandika ngumi kali iliyomtegua bega la kushoto na kumfanya ashindwe
kuendelea na raundi ya pili hivyo mwamuzi Chaku alimaliza pambano hilo kwa
kumpa Chokoraa ushindi wa Knock Out 'KO'.
Akizungumza
na Championi Jumatatu, Puly alisema katika pambano hilo bahati haikuwa yake
lakini akipona bega lake ataendelea kujifua ili arudiane na mpinzani wake huyo.
Naye, Khalid
Chokoraa alijisifia kuwa ni mazoezi makali aliyofanya na sasa anataka mpinzani
mwingine katika uzito wake.
0 COMMENTS:
Post a Comment