MBELWA AKISAIDIWA KUREJEA ULINGONI, ALILALAMIKA KUCHANWA NA NYILAWILA KWA MAKUSUDI AKIDAI ALIMPIGA KICHWA. |
Pambano la ndondi kugombea mkanda wa ubingwa wa UBO, kati ya bondia
Karama Nyilawila na Said Mbelwa lililofanyika usiku wa kuamkia jana (Jumapili)
Ukumbi wa Friends Corner Hotel, Manzese jijini Dar es Salaam, lilikatishwa
kutokana na kuibuka varangati.
NYILAWILA BAADA YA KUPIGWA CHUPA |
Damu ndiyo lilikuwa gumzo baada ya Mbelwa kuchanika kwa madai Nyilawila
alimpiga kichwa lakini Nyilawila naye akapigwa chupa na shabiki wa mpinzani
wake.
Hali hiyo ilisababisha ngumi hizo ziendelee nje ya ulingo hata hivyo,
wahusika wakiwemo wapambe wao waliwahi na kuwaamua na ndiyo ukawa mwisho wa
pambano katika raundi ya sita.
Katika raundi ya tatu, tano
na sita, Nyilawila alimsukuma Mbelwa kwa makonde yaliyompeleka chini lakini
bondia huyo alisimama na kuendelea.
WAKICHAPANA KABLA YA VURUGU KUZUKA. |
Raundi la sita ilipoanza Mbelwa alimvurumishia Nyirawila Masumbwi mazito
mfululizo hali iliyomfanya bondia huyo ajisalimishe kwa kumkumbatia ili
kujiokoa lakini katika tukio hilo alimgonga Mbelwa kwa kichwa juu ya jicho na
kuanza kuvuja damu.
Mbelwa alilalamikia tukio
hilo na kusema ni la makusudi hali ilisababisha waendelee kuzichapa kwa
kukamiana zaidi na kuzisahau sheria za mchezo.
Katika hali ya kukamiana Mbelwa alimbana Nyilawila kwenye kamba na
kumtupia makonde mazito mfululizo na kumtoa nje ya ulingo na kuamua kumfuata
nje ya ulingo na kuendelea kuchapana nae.
Tukio hilo lilisababisha vurumai kubwa na kusababisha mwamuzi Ruta
kuvunja pambano na kukimbia. Mwamuzi huyo na majaji wake wakikimbia hovyo kila
mmoja njia yake gazeti hili lilimkimbiza mwamuzi huyo na kumkamata akitaka
kuvuka barabara ya Morogoro kusalimisha uhai wake.
"Hapa hapafai wataniona hawa, twende tukaongelee kule mbele ona
lile kundi kubwa nahisi linatufuata," alisema Ruta.
"Nimelivunja raundi ya nane lakini tayari Nyilawila alikuwa
akiongoza kwa pointi kwa mujibu wa majaji wangu. Omary Yazidu, Pembe Ndava,
Robert Kasiga na Robert Kasiga
walimpa Nyilawila ushindi wa pointi 68-63, 69-62 na 69-62," alimaliza
kusema mwamuzi huyo.
fin.
0 COMMENTS:
Post a Comment