Uongozi wa Yanga umesema haujamuacha
kiungo mkabaji, Athumani Idd ‘Chuji’.
Hiyo ni siku chache tangu kuwepo kwa
taarifa za kiungo huyo kuachwa baada ya pendekezo la kocha Hans van der Pluijm raia wa Uholanzi ambaye alisisitiza mkongwe huyo atemwe.
Katibu Mkuu wa Yanga, Beno Njovu, alisema Chuji bado ni mchezaji wao mwenye mkataba
wa kuichezea timu hiyo.
Njovu alisema hadi hivi sasa, hakuna
mchezaji yeyote watakayemuacha kwa wale wote wenye mikataba mirefu ya kuendelea
kuichezea Yanga.
“Hizo zote zinazozungumzwa ni tetesi
na siyo habari rasmi kutoka kwa viongozi, Yanga haina mpango wa kumuacha
mchezaji yeyote mwenye mkataba na Yanga.
“Yanga hivi sasa ipo kwenye mazungumzo
na baadhi ya wachezaji kwa ajili ya kuwasajili kwenye msimu ujao, ninaamini
yakiendelea vizuri haraka tutawasajili,” alisema Njovu.
0 COMMENTS:
Post a Comment