Hatimaye yametimia, Kanye West na Kim Kardashian wamefunga ndoa ya aina yake nchini Italia.
Ndoa iliyohudhuriwa na nyota kibao wa muziki na filamu, kasoro Jay Z na Beyonce ambao ni washikaji wakubwa wa Kanye.
Lakini kila kitu kilikwenda katika mfumo wa aina yake na burudani za kila aina.
Hiyo ni ndoa ya pili ya Kim ambaye mwaka 2011 aliolewa na Kris Humphries kabla ya kila mmoja kuchukua time yake.
Kwa sasa Kim na Kanye wana binti mwenye umri wa miezi 11 anayejulikana kwa jina la North.
Maana yake mwanadada huyo mrembo atajulikana kwa jina la Kim kardhashian West. Kila la kheri.
0 COMMENTS:
Post a Comment