Aliyekuwa beki wa Simba, Shomari Kapombe, amewataka Watanzania
kumsamehe kutokana na kiwango cha chini alichoonyesha katika mchezo wa
kimataifa dhidi ya Zimbabwe.
Stars ilivaana na Zimbabwe kwenye mchezo wa kutafuta tiketi ya
kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwakani nchini Morocco.
Katika mechi hiyo iliyofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar
es Salaam, Kapombe alionyesha kiwango cha chini wakati alipokuwa akiitumikia
timu ya taifa (Taifa Stars), jambo ambalo liliwafanya baadhi ya mashabiki kumpigia
kelele kila wakati.
Kapombe amesema kuwa katika mechi hiyo hakucheza vizuri kama
ilivyokuwa zamani akiwa na kikosi
cha Simba na hiyo ni kutokana na kuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu.
Alisema kutokana na hali hiyo, anaomba wapenzi wa soka hapa nchini
wamsamehe kwa hilo ila anaamini kuwa siku chache zijazo atakuwa fiti zaidi na
kurudi katika kiwango chake kama ilivyokuwa zamani.
“Hata mimi niliona kuwa sikucheza vizuri katika mechi hiyo,
nadhani ni kwa sababu nimekuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu bila ya kucheza.
“Hata hivyo, namshukuru Mungu kwani pamoja na hali hiyo
nilijitahidi sana ila nawaomba wapenzi na mashabiki wa soka hapa nchini
kunisamehe kwa yote yaliyotokea siku hiyo, ila naamini kuwa muda mchache ujao
nitarejea katika kiwango changu cha siku zote,” alisema Kapombe.
Katika mechi hiyo iliyofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar
es Salaam, Taifa Stars iliibuka na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na John
Bocco.
0 COMMENTS:
Post a Comment