May 21, 2014



Mdhamini wa klabu ya Simba, Hamisi Kilomoni, amesema atakuwa tayari kuongozwa na kiongozi yeyote atakayeshinda lakini  wagombea watambue kuongoza soka si jambo rahisi kwani wanatakiwa kujipanga na wawe wavumilivu katika kuongoza.


Beki huyo ambaye aliwahi kuichezea klabu hiyo miaka ya nyuma na kwa sasa ni mmoja kati ya wajumbe wa bodi ya udhamini na mali zisizohamishika ya klabu hiyo, ameyasema haya ikiwa ni tahadhari kwa wahusika.

Beki huyo wa zamani amesema atakuwa tayari kuongozwa na yeyote lakini wagombea watambue kuongoza soka si jambo la kubeza hata kidogo hivyo wajipange inavyotakiwa.

Kilomoni alisema  hawezi kusema fulani apite kwani atakuwa anakosea kwa sababu yupo pale klabuni kutunza mali za klabu hiyo, hivyo kiongozi atakayekuja kuiongoza Simba atakuwa tayari kufanya naye kazi.
“Mimi kiongozi atayechagulia Simba kuongoza sina tatizo naye lakini wagombea waliojitokeza watambue kwamba uongozi wa soka si jambo rahisi ni gumu unahitaji kupigana kuwa na uvumilivu na hekima inatakiwa kutumika ili kuweza kuongoza.
“Ingawa mwaka huu wagombea wameamka, tofauti na nyuma, ambapo wengi wamejitokeza katika kuwania uongozi katika klabu, hiyo ni changamoto lakini lazima waitendee haki Simba kwa kuijenga si kujinufaisha,” alisema Kilomoni.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic