May 21, 2014



Nahodha na beki wa kati wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, ametamba kuwa ujio wa kiungo wao mpya, Said Juma, ni furaha kubwa klabuni hapo.


Kauli hiyo ameitoa beki huyo ikiwa ni siku moja baada ya kiungo huyo aliyetokea Pangani inayoshiriki Ligi Kuu ya Zanzibar kusaini mkataba wa miaka miwili na timu hiyo.

Imekuwa ikielezwa kuwa Juma atakuwa mbadala sahihi wa kiungo wa zamani wa timu hiyo, Frank Domayo, aliyetimkia Azam FC.

Cannavaro anasema anaujua vizuri uwezo wa kiungo huyo ndani ya uwanja, hivyo pengo la Domayo halitaonekana katika kikosi chao kinachojiandaa na Kombe la Shirikisho Afrika.
Alisema anajua uwezo wa Domayo ndani ya uwanja, lakini kwa upande wake, Said ni bora zaidi ya kiungo huyo aliyetimkia Azam FC.
“Tofauti na kocha kupendekeza, pia mimi nilitoa mapendekezo ya kusajiliwa kwa Said baada ya kuridhishwa na kiwango chake tukiwa kwenye kambi ya Stars, Tukuyu Mbeya, tukijiandaa na mechi dhidi ya Zimbabwe,” alisema Cannavaro.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic