Kiungo mkabaji wa Simba, Jonas Mkude, amesema hana mpango wa
kuhama klabuni hapo na kujiunga na timu za Azam au Yanga, kwani anaheshimu
mkataba alionao na timu hiyo.
Mkude ambaye ni nguzo muhimu katika timu hiyo ya Msimbazi katika
eneo la kiungo, amekuwa akihusishwa na tetesi za kuihama Simba kwa kipindi hiki cha kuelekea dirisha la
usajili kujiunga na timu hizo mbili za hapa nchini.
Mkude alisema kwa sasa wala hajafikiria mpango wa kuhama na haitatokea
kwa kipindi cha karibuni, kwani maisha ya klabuni hapo ameyazoea.
“Sina mpango wa kujiunga na Azam wala Yanga, kwani nimezoea maisha
ya klabuni kwangu kuanzia uongozi hadi makocha na napata thamani kubwa hapa,
kwa hiyo nasema hizo timu mbili zisiwaze kupata saini yangu kwa kipindi hiki,” alisema
Mkude.
0 COMMENTS:
Post a Comment