MKURUGENZI MTENDAJI WA BIN SLUM TYRES, BIN SLUM AKIONYESHA JEZI ZITAKAZOTUMIWA NA NDANDA FC KATIKA LIGI KUU BARA ZIKIWA NA CHATA YA VEE RUBBER.
Kampuni ya Binslum Tyres Limited imeweka rekodi
mpya katika soka nchini baada ya kuingia mkataba na timu ya tatu inashiriki
Ligi Kuu Bara.
Leo kampuni hiyo imeingia mkataba wa mwaka
mmoja na Ndanda FC ya Mtwara kwa ajili ya kuidhamini katika kuelekea msimu ujao
wa Ligi Kuu Bara.
Maana yake Binslum Tyres sasa itazidhamini timu
tatu za Ligi Kuu Bara ambayo ni rekodi kwa kampuni binafsi kudhamini timu tatu
tofauti, kutoka mikoa mitatu tofauti na yote mitatu kutoka nje ya Dar es
Salaam.
Kampuni nyingi zimekuwa zikivutiwa kuzidhamini
timu za soka kutoka mkoani Dar es Salaam, lakini Binslum Tyres imeleta
mapinduzi.
Huo ni udhamini wa tatu kwa kampuni hiyo kwa
timu shiriki za ligi kuu, nyingine ni Mbeya City na Stendi United iliyopanda
daraja kwa ajili ya msimu ujao.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa
kampuni hiyo, Nassor Bin Slum alisema kuwa udhamini huo umegharamia kiasi cha
shilingi milioni 50 kwa kipindi hicho.
Binslum alisema, lengo la kudhamini timu hizo
ni kujiweka pamoja na wateja wao ambayo kiasi kikubwa yamefanikiwa kwa kiwango
kikubwa kutokana na kuanza udhamini wao Nyanda za Kusini, Nyanda za Kaskazini,
Nyanda za Kati, Zanzibar na Pemba.
Awali Binslum Tyres ilikuwa ikijotolea kuisaidia Coastal
Union ambayo mkurugenzi wake ni shabiki mkubwa wa klabu hiyo.
|
0 COMMENTS:
Post a Comment