Kocha Mkuu wa timu ya
taifa ya Hispania, Vicente del Bosque amesikitishwa na kitendo chake cha kumtoa
mshambuliaji David Villa wakati wa mechi dhidi ya Australia.
Mechi hiyo iliyokuwa ya
mwisho kwa Hispania kwenye Kombe la Dunia, pia ilikuwa ya mwisho kwa ya
Hispania ambayo imefungwa mechi mbili lakini ilikuwa mechi ya mwisho ya Villa
lakini kocha huyo hakujua.
“Nimesikitika kwa kuwa
sikujua kama ni mechi ya mwisho ya Villa, tulikuwa tumeyumba kidogo kwenye
kiungo nikaona ni sahihi kumuongeza Mata.
“Lakini baada ya Villa
kutoka, aliangua kilio pale kwenye benchi, nilipotaka kujua ni kulikoni,
nikaambiwa kuwa ni mechi yake ya mwisho akiwa na jezi ya Hispania, hakika
sikujua,” alisema del Bosque.
Villa ambaye ameondoka
Atletico Madrid baada ya kutwaa ubingwa wa Hispania, sasa anakipiga nchini
Marekani na alitangaza baada ya Kombe la Dunia, atastaafu timu ya taifa lakini
del Bosque akasahau.
0 COMMENTS:
Post a Comment