Kocha
Mkuu wa Simba, Zdravko Logarusic amehama nchini kwake Croatia kwa muda.
“Najua
nikirudi Simba kutakuwa na kazi nyingi sana, kuna mambo kadhaa ya kufanya hivyo
nahitaji kupumzika kwa sasa.
“Nataka
nikirudi tu Croatia, kama nitakuwa narudi Simba basi niwe katika hali nzuri ya
kukimbizana,” alisema akiwa nchini kwenda Bosnia and Herzogovina.
Simba
ilimpa Loga dola 8,000 kama ‘kishika uchumba’ ili asisajili katika kikosi
kingine chochote wakati wanaendelea na usajili.
Lakini
katika kipindi hiki, tayari kamati ya usajili chini ya Zacharia Hans Poppe
imeishaanza usajili na kuna taarifa ndani ya siku chache Logarusic atarejea.
0 COMMENTS:
Post a Comment