Mfadhiri wa zamani wa Simba, Azim Dewji ameonyesha kuwa mwenye furaha kubwa kutokana na kutemwa kwa Michael Wambura.
Hivi karibuni, Wambura alikata rufaa TFF kupinga hatua ya Kamati ya
Uchaguzi ya Simba ambayo ipo chini ya mwenyekiti Dk Damas Ndumbaro kumuengua
katika mchakato huo kwa kosa la kufanya kampeni kabla ya muda uliopangwa.
Dewji amesema kuwa, sasa wana
matumaini makubwa ya kupata viongozi sahihi watakaoiongoza Simba kwa mafanikio
makubwa.
Alisema Wambura ni mmoja kati ya watu wenye uwezo mkubwa wa
kutawala, lakini kwa wakati huu hakuwa chaguo sahihi kwa Simba na kuongeza
kuwa, yote yaliyotokea juu yake anatakiwa kuyapokea kama changamoto.
“Maamuzi hayo ya TFF, tumeyapokea kwa mikono miwili na huu ndiyo
wakati wa sasa kuimarisha Simba, Wambura anatakiwa kukubaliana na hali hiyo na
kuzichukua kama changamoto kwake.
“Nikiwa kama mmoja wa wajumbe wa Friends of Simba, kwa upande wetu
hatuna chuki na Wambura na tutaendelea kushirikiana naye kwa kila jambo akiwa
kama mwanachama mwenzetu wa Simba,” alisema Dewji.
0 COMMENTS:
Post a Comment