Wanachama wachache wa Simba wanaomuunga mkono aliyekuwa
mgombea wa urais, Michael Wambura, wamefunguka kuwa hawajafanya kazi yoyote
wala kufika maofisini kwao badala yake kila siku kufanya mikutano na vikao
kujadili hatima ya ‘rais’ wao huyo.
Wakizungumza na Championi Jumamosi, wanachama
hao walisema wamekuwa watu wa kufanya vikao na mikutano kuijadili kamati ya
Ndumbaro ambayo imemuondoa Wambura kuwania nafasi hiyo.
“Mfano ni mimi hapa, sijafanya kazi yoyote ile
tangu rais wetu aanze kusakamwa. Hii yote ni Ndumbaro na Friends of Simba (FOS)ambao
wamepanga kummaliza Wambura, lakini nasema lazima haki itendeke ikiwezekana
tutaenda mahakamani.
“Julio na Aveva wote
walijinadi kwenye vyombo vya habari, iweje Wambura ndiye asakamwe?” alihoji
mmoja wa wanachama Tawi la Mpira na Maendeleo, Upanga Magharibi.
Hata hivyo, Aveva na
Wambura wote walionywa awali baada ya kubainika wamefanya kampeni. Baadaye Wambura
akarudia.
Pamoja na wengi wanaomuunga
mkono Wambura kuwa wanailaumu kamati ya uchaguzi ya Simba, lakini kamati
iliyothibitisha kuwa kweli alipiga kampeni ni ile rufaa ya TFF.
0 COMMENTS:
Post a Comment