Mwenyekiti wa Matawi ya Klabu ya
Yanga, Mohammed Msumi, amewataka watani wao wa jadi, Simba kuwa makini na fitna
zinazoendelea katika mchakato wa uchaguzi mkuu ambao unatarajiwa kufanyika Juni
29, mwaka huu.
Msumi amesema kwa
sasa wanachama wa timu hiyo wanatakiwa wakae pamoja ili wakubaliane kuliko
kuruhusu fitna ambazo hazina faida yoyote kwao.
“Vizuri sheria zikafuatwa, kama kuna mtu amechinjiwa baharini na anaona ni haki, basi akae kimya badala ya kuendeleza malumbano kupindukia, si sahihi wataimaliza timu yao," alisema.
0 COMMENTS:
Post a Comment