Klabu ya Yanga imetoa nafasi ya
mashabiki wake kuona michuano ya Kombe la Dunia katika mazingira mazuri.
Katibu Mkuu wa Yanga, Beno Njovu amesema
mashabiki na wanachama wa Yanga wamepewa nafasi ya kuangalia michuano ya Kombe
la Dunia kupitia ukumbi wa sinema wa Quality Centre uliopo jijini Dar es
Salaam.
Akizungumza na SALEHJEMBE, Beno alisema
wameamua kufanya hivyo kwa kuwa mazingira ya eneo hilo ni mazuri na ‘screen’ ni
kubwa hivyo wataona mpira kama wako uwanjani.
“Unajua wataona mpira kwa hali nzuri zaidi
kwa maana ya mazingira lakini mfumo wa kuonyesha ni HD, picha zinakuwa katika
kiwango cha juu sana na mtu atajihisi utafiriki yuko Brazil.
“Lengo ni kuwakutanisha pamoja ili
wafurahi huku wakiangalia mpira, hivyo mechi zote zikiwemo zile zinazoanza saa
saba usiku zitaonyeshwa pale, bure,” alisema Njovu na kuongeza.
“Labda nisisitiza, mashabiki wa Yanga na
wanachama tumewaalika kufika na kujumuika. Lakini tunawakaribisha na wapendi
wengine wa mpira wajumuike kwa kuwa soka ndiyo mchezo unaoweza kuwakutanisha
watu kwa pamoja.”
Ndani ya jengo la Quality Centre kuna
majumba matatu ya kuonyeshea filamu na kubwa kuliko yote lina uwezo wa kuchukua
watazamaji 200.
Njovu alisema watakuwa wakifungua
majumba mengine ya kuonyeshea filamu kama idadi ya mashabiki itakuwa kubwa
sana.
Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa klabu kutoa ofa kwa
mashabiki wake kushuhudia michuano ya Kombe la Dunia katika sehemu nzuri.
0 COMMENTS:
Post a Comment