Unaweza
kusema kelele zitapungua, ile timu yenye stori nyingi ya England imetolewa
kwenye Kombe la Dunia.
Mabao
mawili ya Luis Suarez yametosha kuiadhibu England na Uruguay imesonga mbele kuwania
kupata pointi sita katika mechi ijayo, kwa kuwa ya kwanza walipoteza kwa mabao
3-1 dhidi ya Costa Rica na sasa wameibutua England kwa mabao 2-1.
Bao
pekee la England lilifungwa na Wayne Rooney, lilikuwa ni la kusawazisha lakini
Suarez akapachika la pili na kumaliza kazi.
Suarez
ndiye mfungaji bora wa Ligi Kuu England akiwa na mabao 31, hivyo haikuwa shida
kwake kuisambaratisha ngome ya England.
England
imepoteza mechi ya pili mfululizo na sasa inakuwa moja ya timu maarufu
zilizoaga mapema kabisa michuano hiyo.
Hapana Saleh, England wataaga rasmi endapo Costa Rica watashinda. Ila huenda wakapita endapo Italy itazichapa Costa Rica na Uruguay huku England iichape Costa Rica mechi ya mwisho angalau 2-0. Natamani Costa Rica wavuke.
ReplyDelete