Kama ilivyoandika blog hii, Kocha Marcio Maximo
ametua nchini tayari kuanza kazi ya kukinoa kikosi cha Yanga.
Kocha huyo wa zamani wa Taifa Stars ametua
akitokea kwao Brazil kupitia Afrika Kusini.
Maximo amekuwa katika mazungumzo ya takribani mwezi mmoja na nusu na Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji ambaye baadaye alipiga pasi ya mzigo huo kwa makamu wake, Clement Sanga.
Tayari Maximo ambaye ametua nchi na msaidizi wake, wote wawili wamesaiini mkataba wa miaka miwili.
kiungo aitwaye Coutinho, yeye ameshindwa kutua nchini na anatarajia kuwasili kesho au keshokutwa kuungana na wenzake.
Wakati anawasili leo alionekana ni mwenye furaha kubwa na alipokelewa na mashabiki wengi wa Yanga ambao walijitokeza uwanjani hapo.
Wakati anatoka akiongozana na walinzi wakiwemo askari polisi, Maximo alionekana ni mwenye furaha, aliwapa mikono mashabiki wa Yanga na alipowapungia mkono walishangilia kwa nguvu kuonyesha wanamkaribisha.

0 COMMENTS:
Post a Comment