Uongozi wa Klabu ya Yanga, umesema kuwa usajili wa Kocha Mbrazili, Marcio Maximo lazima
ufanywe kwa kutumia ripoti ya aliyekuwa Kocha Mkuu wa timu hiyo, Mholanzi, Hans
van Der Pluijm.
Mbrazili
huyo anatarajiwa kutua siku yoyote kwa ajili ya kukinoa kikosi hicho kinachotarajiwa
kushiriki Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho Afrika.
Katibu Mkuu wa timu hiyo, Beno Njovu, alisema kuwa
Pluijm ndiyo anajua upungufu wa kikosi hicho, hivyo lazima kocha atakayekuja
kuifundisha timu hiyo, atumie ripoti yake.
Njovu
alisema kikubwa wanachohofia ni kujaza wachezaji wengi katika nafasi moja kama
ilivyojitokeza kwenye msimu uliopita, lengo timu hiyo ifanye vizuri katika
msimu ujao.
Aliongeza
kuwa, kikosi chao hakihitaji maboresho makubwa, zaidi ni kuongeza wachezaji
watano katika usajili wa msimu ujao, usajili utakaowahusisha profesheno na
wazawa.
“Usajili
wa timu siku zote unafanywa na kocha aliyekuwa na timu katika msimu wa ligi,
yeye ndiye aliyeona upungufu wa kikosi chake, hivyo lazima ripoti yake
tuiheshimu kwa kuifanyia kazi.
“Huyo
kocha mpya kama akija atakabidhiwa ripoti hiyo na katika ripoti hiyo ya
usajili, kama kuna mchezaji anamfahamu na angependa kumsajili basi haraka
tutamsajili.
“Kati
ya nafasi ambazo zinahitajika kufanyiwa marekebisho ni safu ya beki wa pembeni
namba tatu, kiungo na mshambuliaji mwenye uwezo wa kufunga,” alisema Njovu.
0 COMMENTS:
Post a Comment