Babu Walter Ferreira,
63, ndiye aliyefanya kazi kubwa kuhakikisha mshambuliaji nyota wa Uruguay, Luis
Suarez anarejea uwanjani.
Kitu kizuri zaidi
Ferreira aliamua kuahirisha kwenda kwenye matibabu ya kansa na kuhakikisha
anamsaidia Suarez acheze mechi dhidi ya England.
Ferreaira ambaye ni daktari wa viungo alikuwa akimtibu Suarez ikiwa ni pamoja na kusimamia mazoezi yake binafsi kuhakikisha anakuwa fiti.
Muda mwingi, Suarez alikuwa anafanya mazoezi binafsi akiwa chini ya Ferreira ambaye alikubali kuyaweka maisha yake hatarini kuacha kwenda kupata matibabu ya kansa na kuhakikisha Suarez anakuwa fiti.
SUAREZ NA FERREIRA WAKIWA MAZOEZINI |
Katika mechi hiyo
Suarez alikuwa shujaa na kufunga mabao mawili yaliyoing’oa rasmi England yenye
maneno mengi kwenye michuano hiyo ya Kombe la Dunia.
Suarez alifanyiwa
upasuaji wa goti takribani mwezi mmoja na kukawa na hofu kuwa huenda asicheze
mechi hiyo.
Mechi ya kwanza
Uruguay walikuwa wamepoteza, hivyo walikuwa wanahitaji msaada mkubwa wa Suarez
na Ferreira ndiye alifanya kazi hiyo.
0 COMMENTS:
Post a Comment