Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya
Simba, Dokta Damas Daniel Ndumbaro amefichua siri na kusema yeye ni mwalimu wa
Michael Richard Wambura.
Ndumbaro amesema Wambura ni mwafunzi wa
sheria mwaka wa kwanza katika Chuo Kikuu Huria jijini Dar es Salaam ambako yeye
ni mwalimu.
“Sasa hapa nani atamfundisha mwenzake
sheria, mimi ni mwalimu naye ni mwanafunzi. Mimi ndiye ninayeweza kumfundisha
yeye.
“Najua uwezo wa Wambura darasani,
lakini suala la kimaadili tu ndiyo linazuia kusema kwenye vyombo vya habari.
“Wambura anasema ananipa nafasi ya
kwenda kusoma, lakini nashangazwa na hilo, mimi ni dokta nina PhD. Hilo ndilo
darasa la mwisho duniani.
“Kama ni uprofesa, basi sitawiki kukaa
darasani, hivyo yeye ndiye anapaswa kusoma.
“Nimesikia anasumbuka ada, basi hana
haja ya kunilipia mimi na badala yake apambane kujiendeleza yeye ambaye bado
yuko shule,” alisema Ndumbaro.
Wambura alihoji PhD ya Ndumbaro akidai
alifanya mambo kwa kubabaisha hadi kufikia kumsimamisha.
Lakini leo, Ndumbaro amesema asingeweza
kujibu suala hilo lakini kwa kuwa Wambura aliishambulia kamati na yeye binafsi,
hivyo wameamua kujibu.
“Mimi nilifikiri Wambura angejibu hoja,
kwa kuwa yeye alitakiwa kukata rufaa bila ya kuitukana kamati.
“Kwa mtu mwenye akili timamu,
asingefanya hivyo, badala yake angekata rufaa na kuwasilisha hoja zake. Hapa
tuna barua zake anakili kuondolewa uanachama.
“Lakini yeye amesimamishwa uanachama
wake, anaomba kurejeshwa. Sasa anakataa vipi,” alisema Ndumbaro ambaye ni
mwanasheria na wakili maarufu nchini.
0 COMMENTS:
Post a Comment