Kabla ya
kuanza msimu ujao, tayari kampuni hiyo imesaini mkataba wa kuzidhamini timu za
Ligi Kuu Bara.
Ilianza na
Mbeya City, mkataba wa miaka mitatu wenye thamani ya Sh milioni 360, si mchezo.
Ikaibuka
tena ikasaini mkataba wa Sh milioni 50 kwa mwaka na Stand United ya Shinyanga.
Nimesikia
huenda ikasaini na timu nyingine tena ya Ligi Kuu Bara. Ningekuwa Mwingereza
ningesema: “What a support.”
Hata kama
inatafuta kujitangaza, lakini Bin Slum Tyres imeonyesha mapenzi makubwa kwenye
mchezo wa soka, kudhamini hadi timu iliyopanda daraja.
Timu kuwa
na nguvu kifedha ni kuongeza ushindani wa mchezo huo na kuusaidia kukua.
Hivyo
nikasema wanaopenda soka, wanaweza kwenda kununua bidhaa za Bin Slum ili
kampuni hiyo ione haikukosea kuingia kwenye soka ili iendelee kudhamini, maana
yangu hivi isije ikakimbia maana inahitajika.
Leo
asubuhi, Mwenyezi Mungu kanijaalia afya njema, nimekwenda kwa Bin Slum kununua
matairi pamoja na betri.
Matairi
nitaweka kwenye gari moja, betri kwenye gari jingine, lengo hapa si kutaka
kukutaarifu nina gari zaidi ya moja, badala yake kukuonyesha nilichoandika si
maneno tu, badala yake hata vitendo.
Nimeanza,
ninaamini wengine wanaopenda mchezo wa soka, iwe kutokea mkoani Mbeya,
Shinyanga au Dar es Salaam na mikoa mingine waungeni mkono wafanyabiashara
wanaokubali kuingiza fedha zao kwenye soka na kusaidia.
0 COMMENTS:
Post a Comment