Katika kuhakikisha inarejesha heshima yake, mgombea wa nafasi ya
Umakamu wa Rais wa Simba, Swed Nkwabi amesema kuwa cha kwanza atakachokianza
baada ya kuingia madarakani basi ni kurejesha umoja.
Nkwambi alisema, timu zote inajengwa na wanachama hivyo ni vyema
wakaondoa makundi yaliyojitokeza hivi sasa ndani ya timu yenye malengo mabaya
ya kuibomoa Simba.
“Uongozi wa juu uliomaliza muda wake kuiongoza Simba, ulishindwa
kutimiza majukumu vizuri kwa kushindwa kuvunja makundi yaliyokuwa yanajitokeza
na kusababisha umoja kuvunjika.
“Nimesema hivo siyo kwamba uongozi wa juu uliomaliza muda wake
haujafanya mazuri hapana, yapo baadhi ya matatizo yaliyokuwa yanatokea ya
kibinadamu ambayo yalitakiwa kumalizwa na viongozi wa juu kabisa,”alisema
Nkwabi.
Nkwabi ni kati ya wagombea wanaopewa nafasi ya kutwaa hiyo ni Nkwabi
ambaye alikuwa jembe wakati wa uongozi uliopita.
Nkwabi pia alikuwa mmoja wa mhimili katika safu ya Simba kwenye
uongozi uliopita.
0 COMMENTS:
Post a Comment