AVEVA (KULIA) AKIZUNGUMZA AKIWA NA DALALI. |
Mgombea wa Urais wa
Simba, Evans Aveva amesema kuwa kama akifanikiwa kushinda nafasi hiyo katika
Uchaguzi Mkuu wa timu hiyo, basi atabakisha Kocha Mkuu wa timu hiyo Mcroatia,
Zdravko Logarusic.
Akizungumza jijini Dar
es Salaam, Aveva alisema ni ngumu kwa timu yao kumuacha kocha wenye mipango kwa
hofu ya kukivuruga kikosi chao.
“Hatutamuacha Logarusic
na badala yake tutaendelea naye katika msimu ujao wa ligi kuu, hatuwezi
kumbadili kocha katika kipindi hichi ambacho tunakiboresha kikosi chetu.
“Hivyo ni vyema
tutakaendelea kwa ajili ya msimu ujao, hata ukiangalia usajili wote tunaoufanya
tunatumia ripoti aliyoikabidhi kwenye kamati ya utendaji,”alisema Aveva.
Aidha katika hatua
nyingine Aveva alisema, kama akifanikiwa kuwa rais, basi atahakikisha
analiboresha jengo lao la klabu lililopo mtaa wa Msimbazi na Kariakoo ili liwe
la kisasa liendane na hadhi ya klabu yao.
Aidha, Aveva amesema
anataka Simba kufanya mambo yake kwa kisasa.
Akasisitiza kuwa katika
mambo ya kisasa moja ni suala la usajili ambalo litakuwa katika mpangilio.
"Simba sasa
haijashiriki michuano ya kimataifa kwa misimu miwili, hivyo lazima kufanya
mambo kitaalamu zaidi, tujipange na kuhakikisha tunashiriki michuano ya
kimataifa.
"Simba ndiyo timu
yenye mafanikio zaidi katika ngazi ya kimataifa, hivyo lazima niirudishe katika
kiwango na haitakuwa kazi lahisi lakini nitapambana," alisema Aveva ambaye
alikuwa ameongozana na Mwenyekiti wa zamani wa Simba, Hassan Dalali.
Aveva anagombea nafasi
ya urais dhidi ya Andrew Tupa ambaye amekuwa kimyakimya.
0 COMMENTS:
Post a Comment