Kila
mpenda mpira hasa watu wa mazoezi angependa kuwa na mwili uliogawanyika kama
ule wa Cristiano Ronaldo.
Unakumbuka
alipofunga bao la nne dhidi ya Bayern Munich kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa
Ulaya, akatunisha misuli, si mchezo.
Lakini
si lahisi kuwa kama yeye, maana taarifa zimevuja kuwa pamoja na mazoezi mengine
huwa analiinua gari aina ya Toyota Prius mara 16.
Lengo
la kufanya hivyo ni kujenga mwili wake zaidi na kweli anaonekana kufanikiwa.
Pia
imeelezwa kuwa Ronaldo amekuwa akifanya yale mazoezi ya tumbo, kulala na kuamka
mara 3,000!
Pamoja
na hivyo anakuwa kwenye mpangilio mzuri wa chakula au diet na anakula zaidi
vyakula vyenye protini na cabohydrates, pia amekuwa akilala kwa saa nane kila
siku.
0 COMMENTS:
Post a Comment