Wachezaji wanne kutoka nchini Ghana wanataka kuja nchini kuichezea Simba katika msimu
ujao wa Ligi Kuu Bara.
Wachezaji
hao, washambuliaji wawili, beki na kiungo mmoja wako tayari kuichezea Simba na
wamefanya mawasiliano na Kocha Zdravko Logarusic.
Akizungumza
kutoka kwao Croatia, Loga ameliambia Championi Jumatatu kuwa Waghana hao wako
tayari lakini amewataka wavute subira.
“Wanataka
kuja kweli kama ulivyoambiwa, karibu wote nimefanya nao kazi katika timu za Ghana
pia ni wachezaji wazuri.
“Lakini
siwezi kukurupuka na kuwaita tu, kwanza ni kuangalia mahitaji ya timu, baada ya
hapo ninaweza kujua cha kufanya.
“Na hata
kama nitafikia kuwa niwaruhusu waje, lazima nijue maendeleo yao, rekodi zao kwa
kipindi hiki. Ndiyo maana nilisema sikuwahi kupendekeza mchezaji yoyote kutoka
Kenya.
“Nasisitiza
suala la wachezaji wan je ya Tanzania bado, ila wako hao na wengine wanataka
kuja, ikifikia, basi nitaifanya kazi hiyo. Sasa bado nasubiri uchaguzi wa
Simba,” alisema Loga.
Simba iko
katika mchakato wa uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika Juni 29, hali
iliyosababisha zoezi la usajili kusuasua.
%%%%%
Yanga yampa
Maximo wachezaji 60
Na Mwandishi
Wetu
KOCHA
anayetarajiwa kujiunga na Yanga kama mambo yatakwenda vizuri, atapewa takribani
wachezaji 60 wawe chini ya himaya yake.
Uongozi wa
Yanga kupitia kamati yake ya mashindano umechukua uamuzi wa kumkabidhi Maximo
timu kubwa pamoja na ile ya vijana chini ya miaka 20.
Uamuzi huo
unatokana na historia ya Maximo ambaye alikuza vijana wengi wakati akiwa kocha
wa timu ya taifa, Taifa Stars.
“Ukiangalia
Maximo ndiye alikuwa na uwezo mkubwa wa kuona kijana ambaye atakuja kuwa
mchezaji bora hapo baadaye. Angalia Jerry Tegete, pia Kiggi Makasi na wengine.
“Hivyo kama
tutamkabidhi timu hizo mbili, maana yake atakuwa na uwezo wa kujua vijana
wanaofanya vizuri na atawapandisha kwenye timu kubwa.
“Au anaweza
kuwa anapendekeza vijana kutoka timu mbalimbali, wanajiunga na timu ya vijana
ya Yanga halafu baadaye wanapandishwa kwenye timu kubwa,” kilieleza chanzo.
Mazungumzo
ya kuhakikisha Maximo anatua nchini au la, yamefikia asilimia 95 na kocha huyo
ameonekana yuko tayari kutoka kwao Brazil na kuja kuanza kazi ya kuinoa Yanga
kwa kuchukua nafasi ya Hans van der Pluijm.
Championi
ilikuwa gazeti la kwanza kuandika kuhusiana na ujio wa Maximo baada ya Yanga
kuanza kufanya naye mazungumzo na wakati huo yalikuwa yamefikia asilimia 90,
sasa yamepanga hadi 95 na huenda katua nchini ndani ya siku chache zijazo.
Kazimoto,
Tegete, Henry wajichimbia Mwanza
Na Mwandishi
Wetu, Mwanza
WACHEZAJI
nyota kutoka katika timu mbalimbali wamerejea mapumzikoni jiji hili maarufu kwa
kuzalisha wachezaji nyota.
Mshambuliaji
wa Yanga, Jerry Tegete, kiungo wa Simba, Henry Joseph na kiungo wa Al Markhiya
ya Qatar, Mwinyi Kazimoto ni kati ya wachezaji walio mapumzikoni jijini hapa.
Wote watatu
walichipukia kisoka mkoani hapa kabla ya kufunga safari na kwenda mikoa ya
Pwani na Dar es Salaam kusaka maisha zaidi.
Wachezaji
hao wamekuwa wakionekana katika mitaa mbalimbali wakiwa na marafiki na ndugu
zao wakiendelea kujivinjali.
Taarifa
zinasema huenda Mrisho Ngassa na Kelvin Yondani, wanaweza kuwasili hapa leo na
kuondoka kesho ili kuiwahi kambi ya timu ya taifa.
Mwanza,
Kigoma na Mbeya ndiyo mikoa inayoongoza kwa kutoa wachezaji wengi nyota katika
soka nchini.
0 COMMENTS:
Post a Comment