Hali ya kutaka kujua kuwa mgombea
wa urais wa Simba, Michael Wambura aliyeenguliwa baada ya kubainika si
mwanachama amerudishwa na kamati ya rufaa ya TFF imekuwa kubwa.
Inaonekana ni hali ya kila mmoja
kutaka kujua kuhusiana na Wambura amerudishwa au la.
Gumzo kwa masaa manne kuanzia saa
10 jioni, imekuwa ni kutaka kujua kuhusiana na Wambura ambaye rufaa yake
ilikuwa inasikilizwa leo.
Lakini taarifa ilizozipata blogu
hii pamoja na kuwa na tetesi ambazo si rasmi kuwa Wambura amerudisha, lakini
ukweli bado mambo ni magumu.
Kamati hiyo ilikuwa ikiendelea
kujadili kuhusiana na suala hilo huku waliopinga nao wanatoa maelezo yao na
Wambura akipewa nafasi ya kujibu.
Chanzo cha kwanza kimesema
Wambura anakaribia kurudishwa, lakini kingine kimeeleza kuwa inaonekana uamuzi
wa kamati ya uchaguzi ya Simba ulikuwa sawa, hivyo unaipa kazi kubwa kamati ya
rufaa kuhusiana na hilo na huenda inataka kupindisha.
Hivyo bado hali ni ngumu na
majibu sahihi bado hayajapatikana na huenda mambo yanaweza yakaendelea tena
kesho.
Lakini uhakika wa kupata majibu
ya kilichojadiliwa na uamuzi ni nini itakuwa kesho.
Bado tunaendelea kufuatilia kujua
kuhusiana na hilo.
0 COMMENTS:
Post a Comment