Wakati harakati za usajili kwa timu za Ligi Kuu Bara zikizidi kushika kasi, uongozi wa
Stand United ya Shinyanga, umejikita rasmi katika harakati za kuhakikisha
unamnasa mshambuliaji wa Yanga, Said Bahanuzi ambaye kwa sasa yupo huru
kujiunga na timu yoyote.
Kocha wa Stand, Athuman Bilal ‘Bilo’, amesema viongozi
wa Stand United juzi Alhamisi walifanya kikao cha pamoja kwa ajili ya kujadili
suala la kumnyakua mshambuliaji huyo aliyejiunga na Yanga misimu miwili
iliyopita akitokea Mtibwa, ambaye kiwango chake kimeshuka ghafla.
“Bado
hatujakamilisha usajili wetu, uongozi unaendelea na utaratibu huo, pia
kuhusiana na Bahanuzi ndiyo kwanza tumeamua kumfungia kazi ili msimu ujao tuwe
naye na njia za kupita tayari jana (juzi), tumezizungumzia katika kikao chetu.
“Ni
matumaini yetu kuwa Mungu akipenda mchezaji huyo tutakuwa naye msimu ujao,”
alisema Bilal.
0 COMMENTS:
Post a Comment