July 7, 2014



Uongozi wa klabu ya Barcelona, umeamua kumtuma mmoja wa madaktari wake kwenda nchini Brazil kuunga na Neymar ambaye ni majeruhi.
Mkurugenzi wa Michezo wa Barcelona, Andoni Zubizarreta amesema wamekuwa na mawasiliano na Shirikisho la Soka Brazil (CBF) kuhusiana na afya ya Neymar.
“Huu ni wakati mzuri wa kuwa naye karibu, daktari wetu atakuwa pamoja na madaktari wa Brazil na kujua maendeleo yake na kama itawezekana kuwa naye mwanzoni mwa msimu wa La Liga au la.
“Tumekuwa na mawasiliano mazuri na CBF, wametuambia anaendelea vizuri na tayari yuko nyumbani,” alisema bosi huyo.
Neymar aliumia katima mechi ya robo fainali ya Kombe la Dunia baada ya kurukiwa na beki Zunuga wa Colombia.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic