Na Eddie Salim
Ijumaa
04/07/2014, Wenyeji Brazil wataikaribisha Colombia katika Robo fainal ya
kwanza. Wabrazil na wanaoipenda Brazil wataelekeza mikono yao juu kusali na
kuomba dua timu yao ishinde.
Kama walivoelekeza siku
waliyocheza na Chile ilipokosa bao la wazi katika dakika za mwisho kabla
ya matuta.
Brazil mpaka sasa
haikuonyesha kiwango chao cha kweli,ila kadiri wanavosonga mbele timu itakua
inapafom uzuri. ila mechi ya Colombia haitakua lelemama kwani mpinzani
ameshinda mechi zake zote nne na ina mfungaji mzuri mno ambaye mpaka sasa
amefunga mabao 5.
Pia mpinzani inacheza
as team, pia siku ya ijumaa watakua hawana presha kama inavyo Brazil. Kwa
mtu yoyote anayefuatilia Brazil anajua wazi kua Brazil wanamtegemea sana
Neymar, ambaye Ijumaa wa Colombia hawatamuachia acheze anavotaka.
Hapa itabidi wenzake
wamtue mzigo kwa hio akina Hulk na Fred watabidi wae tayari kwa kufanya
kazi ya ziada.
Brazil ya mwaka huu haina
jina zito ambalo linawashtua wapinzani wao kama hapo nyuma,hii inatokano
na ukaidi wa Scolari kama alivofanya mwaka 2002 alivokataa mwito wa Raisi
wa Brazil alipotakiwa amchukue Romario,ila wakati ule Brazil ilikua inavifaa
kama Gaucho,Rivaldo na Ronaldo.
Ninavyona angemchukua
mmoja kati ya watatu hawa timu ingekua na uzito na ukali ziada. Kama angekua
supa sub zaidi ya Benard- with my respect- Gaucho angekua
bomba mbele kuliko Jo-with my respect to Jo- au hata Bato nae angesaidia.
angemuingiza mmoja kati
ya hawa pale timu inapo hitaji uzoefu na uwezo.
Mwisho kabisa nnawatakia
mechi nzuri katika robo fainal zote kwani waliofika stage hii ndio wanaoujua
mpira,na waliotolewa wangojee mpaka 2018 kwenye uhai. KILA LA HERI
SELECAO....ABRIGADO BRAZIL!!!!!!!!!
MWANDISHI WA MAKALA HAYA NI MSOMAJI WA BLOG HII.
0 COMMENTS:
Post a Comment