July 11, 2014

NEIVA (KUSHOTO) AKIWA NA BOSI WAKE, MARCIO MAXIMO.


Kocha Msaidizi wa Yanga, Leonardo Neiva, raia wa Brazil, ameanza kujifunza kuzungumza Kiswahili ili apate urahisi wa kuwasiliana na wachezaji wake ambapo asilimia kubwa wanazungumza lugha hiyo.


Neiva alitua nchini wiki mbili zilizopita akiwa na Marcio Maximo ambapo kazi kubwa aliyokabidhiwa ni kuwanoa vijana wa timu hiyo.

Gazeti hili limekuwa likimshuhudia Neiva akipata wakati mgumu kujifunza maneno kadhaa ya Kiswahili katika mazoezi mbalimbali ya timu hiyo ambapo amefanikiwa kuelewa maneno kadhaa.

Baadhi ya maneno ambayo alikuwa akiyatumia mara kwa mara katika mazungumzo yake na wachezaji ni ‘haraka-haraka’, ‘matatizo’ na ‘tuko pamoja’ ambalo hutumiwa zaidi na bosi wake, Maximo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic