July 11, 2014



Mshambuliaji wa Simba, Amissi Tambwe, raia wa Burundi, ameanza kujifua rasmi jana kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao lakini hapohapo akamtupia dongo kiungo mpya wa Yanga, Mbrazili, Andrey Coutinho.


Tambwe alitua nchini juzi usiku na kuamua kuingia mzigoni moja kwa moja kujumuika na wenzake kwenye mazoezi ya gym yanayofanyika Chang’ombe, Dar es Salaam.

Baada ya kumalizika kwa mazoezi hayo, Tambwe amesema amerejea kuendelea na makali yake na yupo fiti kwa ajili ya msimu ujao lakini akaongeza kwamba, hahofii ujio wa Coutinho kwa kuwa anaamini atakuwa na kiwango cha kawaida.

“Kwani Brazil kitu gani, unaweza ukatoka Brazil na ukawa wa kawaida tu, mimi simjui na sijawahi kumuona lakini hawezi kusumbua kichwa kwa sababu si wote wanaotoka Brazil wanajua mpira, cha msingi kama kweli ni mzuri basi tutamuona uwanjani.
“Kama ingekuwa kila Mbrazili ni mzuri na wanajua mpira kuliko wengine wote basi wasingefungwa 7-1 na Ujerumani,” alisema Tambwe.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic