Kamati ya
usajili ya Simba chini ya Zacharia Hans Poppe imeonyesha imepania kweli
kuboresha kikosi baada ya kumalizana kwa asilimia 95 na mshambuliaji hatari
kutoka Kenya.
![]() |
| AKIWA NA LOGARUSIC |
Kiongera ni
kati ya wachezaji walio katika kikosi cha timu ya taifa ya Kenya, Harambee
Stars na Kocha Adel Amrouche amezungumza na Championi JUmatatu na kusema Simba
wakimnasa, watakuwa wamekula Bingo.
“Ni mmoja
wachezaji ambao nimekuwa nikiwaita kwenye kiksoi changu, kama Simba wakimpata
ni mmoja wa wachezaji bora,” alisema Amrouche raia wa Ubelgiji.
Taarifa za
uhakika zinaeleza mchezaji huyo mrefu, mwenye sifa ya mashuti makali,
anatarajia kutua nchini ndani ya siku mbili tayari kusaini mkataba wa kuichezea
Simba.
![]() |
| AKIWA NA MUSOTI |
“Kila kitu
kinakwenda vizuri na kamati ya usajili chini ya Hans Poppe inafanya mambo yake
kwa umakini mkubwa, hivyo Mkenya anakuja kuungana na Simba,” kilieleza chanzo.
“Mazungumzo
yamekwenda vizuri, baada ya Kiongera kutua Dar nafikiri litakuwa ni suala la
kumalizia tu, maana mambo yaliyobaki ni mdogo sana.”
Kiongera
alikuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu Kenya mwaka 2012 wakati akikipiga Gor Mahia
kwa mkopo, mwaka huo ndiyo Kocha Zdravko Logarusic akabeba tuzo ya kocha bora
nchini Kenya.
Taarifa
zinaeleza, Logarusic ndiye aliyembeba Kiongera kutoka KCB kwa mkopo hadi Gor
Mahia na baada ya hapo, wakaanza kukamua pamoja hadi kufikia kubeba ngao ya
hisani na baadaye wakashiriki michuano ya Kombe la Shirikisho.
Pamoja na
Loga, mwingine aliyewahi kufanya kazi na Kiongera ni Donald Musoti na kipa Ivo
Mapunda, sasa wanakutana tena Simba.










0 COMMENTS:
Post a Comment