July 7, 2014

MANJI

Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji ameandika barua kwenda katika makao makuu ya Simba na juu ya bahasha kuna kuna jina, Evans Aveva.


Barua hiyo ya Manji kwa Aveva imetua klabu hapo na kupokelewa na imeelezwa ina ujumbe mzito ambao umeweka historia katika soka nchini katika kipindi hiki.
Ingawa SALEHJEMBE haijapata kopi ta barua hiyo, lakini imeshuhudia bahasha hiyo ambayo inakwenda moja kwa moja kwa 
AVEVA

Aveva ambaye ni Rais mpya wa Simba.
Aveva ameibuka na ushindi wa kishindo dhidi ya aliyekuwa mpinzani wake, Andrew Tupa katika uchaguzi uliofanyika Jumapili iliyopita.

Awali SALEHJEMBE ilielezwa barua hiyo ya Manji kwa Aveva ni kuhusu mambo ya siri, hali ambayo kwa kiasi fulani ilizua hofu kwa baadhi ya mashabiki na wanachama hasa wa Simba, wakitaka kujua mwenyekiti wa watani wao alikuwa anamweleza nini mwenyekiti wao mpya.

Lakini baadaye likapata uhakika kuwa Manji amempongeza Aveva na safu yake yote ya uongozi kwa kuibuka washindi.

“Barua ile ya Manji ni pongezi kwa Rais Aveva, tayari ilipokelewa klabuni na kupelekwa kwake,” kilieleza chanzo.

Manji ameweka rekodi nyingine kwa kuwa katika siku za hivi karibuni haijawahi kutokea kiongozi wa klabu hizo kongwe kutoa pongezi na kuutakia kila la heri uongozi kwa upande mwingine, tena kwa barua.

Taarifa za ndani ya Simba zinaeleza barua hiyo ya Manji, pamoja na pongezi imesisitiza Yanga na Simba zinaweza kushirikiana na masuala ya msingi ili kuboresha uwezo wa kifedha wa timu hiyo.

Lakini Manji akasisitiza kwamba, Yanga na Simba zitaendelea kupambana uwanjani kwa ushindani mkubwa kwa lengo la kuinua kiwango cha soka nchini na maslahi ya klabu hizo kongwe nchini.

Msimu uliopita, Manji akiwa uwanjani mara baada ya Yanga kufungwa, alikwenda kuwapa mikono viongozi wa Simba akiwapongeza kutokana na ushindi huo, halafu akaondoka uwanjani.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic