Makocha wa
zamani wa Yanga, Hans van der Pluijm na msaidizi wake, wameanza kazi ya kuwanoa
wachezaji kutoka mataifa tofauti manne.
Akizungumza
na Championi Jumatatu kutoka nchini humo, Pluijm alisema kadiri siku
zinavyosonga mbele wamekuwa wakizoea mazingira.
“Kama
nilivyowahi kuwaeleza awali, hali ya hewa ya joto kali ilikuwa inatusumbua,
lakini sasa tumezoea,” alisema Pluijm raia wa Uholanzi.
“Lakini sasa
mambo ni mazuri na mazoezi yetu yanakwenda vizuri sana. Tunaendelea vizuri kwa
asilimia kubwa na tunachosubiri ni kuanza kwa msimu.”
Pluijm ndiye
aliyeushawishi uongozi wa Al Shaolah kumchukua Mkwasa ambaye walifanya kazi kwa
ushirikiano mzuri wakiwa Yanga.
SOURCE: CHAMPIONI








0 COMMENTS:
Post a Comment