Tayari timu ya Taifa, Taifa Stars ipo kwenye harakati za mwisho za
kuanza kambi yake leo huko Tukuyu, Mbeya kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wao
dhidi ya Msumbiji huku sababu ya kuwapeleka mkoani humo ikitajwa ni kuyaepuka
magonjwa ya Malaria na Dengue.
Bilie Haonga
amesema kuwa wameamua kufanya hivyo ili kuweza kuhakikisha afya za wachezaji
wao zinakuwa imara kwa kuepuka magonjwa kama Malaria na Dengue.
Bilie alisema kuwa
wameiepuka Dar kutokana na hali ya hewa ilivyo kwa sasa hivyo kuna uwepo wa
asilimia nyingi za kupata Malaria na Dengue kwa kipindi hiki kutokana na Dar
kuwepo kwenye Ukanda wa Bahari.
“Tunaenda Tukuyu kwa sababu nyingi, kwanza tunazingatia afya za
wachezaji kwa kuwaepusha na magonjwa mengi kama Malaria na Dengue
inayosababishwa na hali ya hewa ilivyo kwa sasa hasa ukizingatia Dar ipo kwenye
usawa wa Ukanda wa Bahari.
“Lakini kwa sasa hali ya kikosi ni nzuri, kasoro Jonas Mkude na Himid Mao ambao wanafanyiwa vipimo
vya MRA kutokana na kuumia,”
alisema Bilie.
Kwa upande wa kocha wa Stars, Mholanzi Mart Nooij alipokuwa akizungumza na Waandishi wa
Habari jijini Dar jana alikuwa akiulizwa maswali kuhusiana na maandalizi ya
mchezo huo alitoa majibu ambayo yalishangaza.
Mfano wa maswali aliyokuwa
akiulizwa ni pamoja na, Je amejipanga vipi kuwakabili Msumbiji? Ambapo alisema:
“ Kikubwa ninachoomba ni mashabiki wajitokeze kwa uwingi kuhakikisha wanakuja
kuisapoti timu, wafike idadi hata ya watu elfu 70.”
Ingawa soka ni mchezo ambao upo tofauti na matokeo, matarajio ya michezo
mingine huku akisema kuwa lolote linaweza kutokea katika mchezo huo na kwamba
ni sawa na Tenisi katika michuano ya French Open kwamba hata Rafael Nadal
ambaye ni mchezaji mkubwa huwa anafungwa na wadogo.
Aliulizwa jingine kuwa, anawazungumziaje Msumbiji ambao alikwenda
kuchukua CD ili kuweza kutumia pindi akifundisha wachezaji wake akajibu;
“Nilikwenda Msumbiji kwa sababu niliwahi kuishi kule kwa hiyo nilikwenda
kuangalia akaunti yangu ya benki na sio vingine.
Vipi kuhusiana na Kombe la Dunia?; “Siwezi kuanza kuzungumzia masuala ya
haya badala ya kuangalia mambo yaliyopo mbele yangu.”
Hata hivyo, Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura alisema kuwa wachezaji
wanaocheza nje wanatarajiwa kuwasili nchini siku tano kabla ya mchezo na
wamekwisha watumia taarifa wote watatu ambao ni Mwinyi Kazimoto anayekipiga Al
Marikhya ya Quatar pamoja na Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wanaoichezea TP
Mazembe ya DRC.
0 COMMENTS:
Post a Comment