Kocha Mkuu wa Simba, Zdravko
Logarusic amesema Ligi Kuu Bara msimu ujao haitakuwa lahisi au lelemama, lakini
mwisho Simba ndiyo itafanya vizuri.
“Ili tiu ifanye vizuri kuna mambo
mengi sana yanatakiwa kwenda sawa.
“Wachezaji lazima wawe makini na
waelewe tunachokifanya ni nini kwa faida yao nay a timu.
“Pia wajue tunataka ushindi na
mafanikio yatapatikana kwa kila mmoja kuwa na malengo na kufanya kazi yake kwa
asilimia mia.
“Kwa upande wa uongozi, utekeleze
kinachotakiwa kutoka kwa benchi la ufundi na mahitaji muhimu ya wachezaji,”
alisema Logan a kuongeza.
“Naamini ligi itakuwa ngumu sana,
lakini mwisho tutashinda hasa kama tutakwenda kwa mtiririko huo.”
Simba inaendelea na mazoezi yake
ufukweni, pia kwenye Uwanja wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
0 COMMENTS:
Post a Comment