Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limeendesha mafunzo ya matumizi ya tiketi za
elektroniki kwa wadau wa mpira wa miguu mkoani Mbeya.
Mafunzo hayo
yamefanyika jana na leo (Julai 4 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Sokoine, na
kushirikisha wasimamizi wa mechi, viongozi wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa
Mbeya (MREFA) na makatibu na maofisa habari wa klabu za Tanzania Prisons na
Mbeya City.
Wengine
walioshiriki mafunzo hayo ni Meneja wa Uwanja wa Sokoine na msaidizi wake,
wasimamizi wa milangoni (stewards) na waandishi wa habari wa mkoani Mbeya.
Mafunzo hayo yanahitimishwa kesho (Julai 5 mwaka huu)
kwa mechi kati ya Tanzania Prisons na Mbeya City itakayochezwa Uwanja wa
Sokoine kuanzia saa 10 kamili jioni. Kiingilio ni sh. 3,000, na tiketi zilianza
kuuzwa Julai Mosi mwaka huu kupitia M-Pesa, CRDB Simbanking na maduka ya Fahari
Huduma.
0 COMMENTS:
Post a Comment