Taasisi moja
kutoka Uingereza inayohusika na kampeni dhidi ya upangaji matokeo kwenye mpira
wa miguu (match fixing) itafanya uwasilishaji (presentation) juu ya suala hilo
kwa waandishi wa habari za michezo nchini.
Uwasilishaji huo
utafanyika kesho (Julai 5 mwaka huu) saa 11 jioni kwenye hoteli ya Accomondia
iliyopo Barabara Nkrumah jijini Dar es Salaam.
Wataalamu hao wa
kupiga vita upangaji matokeo ambao pia wataelezea jinsi matokeo yanavyopangwa,
jana (Julai 3 mwaka huu) walifanya uwasilishaji wao kwa wachezaji na benchi la
ufundi la timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti
Boys).
Taasisi hiyo yenye kibali kutoka Shirikisho la
Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) katika utoaji elimu ya kubaini upangaji
matokeo, vilevile inatoa elimu juu ya athari zinazopatikana kutokana na
upangaji matokeo.
0 COMMENTS:
Post a Comment