July 4, 2014



Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Mart Nooij, amemuondoa kiungo mshambuliaji wa Yanga, Mrisho Ngassa katika kikosi chake kitakachoivaa Msumbiji.


Sababu kubwa iliyotajwa ni Ngassa kushindwa kuripoti katika kikosi hicho wakati alipoitwa kucheza dhidi ya Botswana kabla ya kuivaa Msumbiji katika kuwania kushiriki Kombe la Mataifa Afrika (AFCON).

Chanzo cha habari kutoka ndani ya benchi la ufundi la Stars, kimesema kuwa Ngassa alikaidi wito wa kocha huyo na kwenda Afrika Kusini kufanya majaribio na Free State Stars ambako alifanya majaribio na kufuzu.

"Kocha ameamua kuachana naye kwa kuwa Ngassa hakwenda Botswana, badala yake alikwenda Afrika Kusini kwenye klabu ya Free State Star kufanya majaribio.
"Hivyo Nooij ameamua kumuondoa kwenye kikosi chake na hatacheza dhidi ya Msumbiji," kilieleza chanzo.

Alipoulizwa Katibu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Selestine Mwesigwa alisema hawana taarifa yoyote juu ya kutokuwepo kambini kwa mchezaji huyo.

"Ngassa hakuripoti kambini, sasa inakuwaje Yanga waseme ameondokea kambini, si kweli, hivyo hatuhusiki lolote kuhusiana na Ngassa," alisema Mwesigwa.

Awali, Yanga walitangaza kutaka maelezo kutoka TFF kwamba Ngassa amekwenda vipi Afrika Kusini wakati walikuwa wakijua yuko kambini.

Lakini baadaye kukaibuka kwa taarifa hizo kwamba Ngassa hakuripoti kambini Botswana.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic