July 4, 2014

UMONYI


Uongozi wa Azam FC umemtema rasmi kiungo wao mshambuliaji Mganda, Brian Umony, aliyekuwa anaichezea timu hiyo msimu uliopita.


Umony alitua kuichezea timu hiyo kwenye msimu uliopita kwa mkataba wa miaka miwili na kuiwezesha Azam FC kutwaa ubingwa wa ligi msimu uliopita.

Kwa mujibu wa chanzo cha habari kutoka ndani ya uongozi huo, kiungo huyo wameusitisha mkataba wake wa mwaka mmoja alioubakiza, hivyo ni mchezaji huru hivi sasa.

Chanzo hicho kilisema, tayari wapo viungo wawili wa kimataifa ambao wametua nchini wakiendelea na majaribio chini ya kocha Joseph Omog.

Kiliwataja wachezaji hao kuwa ni Leonel Saint-Preux kutoa Hait na Gery Epeso aliyekuwa kwenye akademi ya Orlando Pirates ya nchini Afrika Kusini ambaye ni raia wa Congo.

“Umony tumemalizana kwa amani kabisa. Wapo wachezaji wawili hivi sasa wanaoendelea na majaribio, kati ya hao, yule tutakayevutiwa naye atachukua nafasi yake,” kilisema chanzo hicho.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic