Awali ilionekana kama ni kitu kisichowezekana, lakini sasa wachezaji nyota kabisa wa Real Madrid watakanyaga ardhi ya Tanzania.
Wakongwe au magwiji waliowahi kukipiga Real Madrid ambao wana kikosi chao maalum cha Madrid Legends, watatua nchini na kuanza ziara ya siku nne.
Rasmi watu hao watatua Agosti 22 mwaka huu ambapo
watacheza mechi moja ya kirafiki dhidi ya kikosi maalum cha nyota wa Tanzania.
Ziara hiyo ni mwaliko wa kampuni ya Tanzania Sisi ni Nyumbani (TSN),
Mkurugenzi wake mkuu, Farough Baghozah na meneja wa ziara hiyo ni
Dennis Ssebo.
Dennis Ssebo ameiambia SALEHJEMBE kuwa maandalizi
yako safi kabisa, pia ni nafasi nzuri kwa wapenda soka wa nyumbani Tanzania na nchi jirani kupata nafasi ya kuwaona nyota kibao enzi za akina Luis Figo, Zinedine Zidane na wenzao kamaRonaldo De Lima na Carlos, Zinedine Zidane.
“Ninaloweza Kusema ni kwamba, Watanzania wakae tayari kupokea
wachezaji 27 wa zamani wa timu ya Real Madrid na mashabiki 23 kutoka
Hispania wanaokuja kuwashangilia magwiji wao. Kwahiyo jumla tunapokea watu 50
kutoka Hispania kwa ajili ya ziara hii”. Alisema Ssebo.
“Ni ziara ambayo tulifikiria itakuwa fupi, lakini wenzetu kumbe
wameipenda nchi na wanaifahamu, kwahiyo ni ziara ambayo itachukua takribani
siku nne”. Aliongeza.
Ssebo alisema Magwiji hao wataingia nchini Agosti 22 mwaka huu na
watacheza mechi maalumu ya kirafiki Agosti 23 ndani ya dimba la kisasa la
Taifa, jijini Dar es salaam.
“Baada ya mechi wataenda Arusha Agosti 25 kuangalia vivutio vya utalii na
watalala huko. Watalala tena Dar es salaam na kuondoka tarehe 26 ya mwezi wa
nane”.
0 COMMENTS:
Post a Comment